PRIVATE CANDIDATE AND QT NOTIFICATION
education blog ingependa kuwakumbusha watahiniwa wa mitihani ya kujitegemea PCs kuhakiki taarifa zao kabla ya kuingia chumba cha mtihani.
taarifa hizo ni barua ya uthibitisho kutoka baraza la mitihani tanzania (NECTA) ikiwa ina taarifa za kumruhusu mwanafunzi kufanya mitihani fulani. kawaida barua hizo huambatanishwa na:
1. jina la mwanafunzi
2. picha
3. namba ya mtihani
4. muda wa mtihani
5. kituo cha mtihani
n.k
masomo atayofanya mwanafunzi yataonekana kama ifuatavyo:
barua hiyo itaweza kuonekana kama ifuatavyo:
taarifa hizi mwanafunzi yapasa azihakiki kama ni sahihi, kama vile herufi za jina lake pamoja na mitihani aliyochagua kufanya.
education blog ingependa kuwasihi wanafunzi wa QT kufanya mazoezi zaidi katika kuandika, ukizingatia mitihani yao itafanyika ndani ya masaa matatu tu. kwa masomo matano
wanafunzi wa private candidate kufanya mazoezi zaidi katika uandishi wa insha za kiswahili na kingereza ukizingatia ni vipengere vyenye alama nyingi.
MAKOSA KATIKA CHUMBA CHA MTIHANI
si ruhusa kufanya udanganyifu wowote katika chumba cha mtihani, kufanya hivyo ni kosa kisheria, waweza kushtakiwa au kufungiwa kabisa kutofanya mitihani ya necta kwa miaka kadhaa.
wanafunzi wanashauriwa kufanya juhudi binafsi, hii itawajengea uwezo hata wakifika kwenye elimu za juu
maandalizi mema ya mitihani 2015